ALICE KAMANDE – WEWE PEKEE

Nafungua kinywa changu, nikusifu Baba

Umenitendea nimefika sasa hapa

Wewe kweli ni rafiki, Unaniongoza ninapopotea

Upendo wako niufananishe na nani baba

Taabu nyingi kweli nilipitia

Hadi nikajipata nikikushuku

Sikujua mpango wako kwangu Baba

Ulijua yote nikiyapitia

Mkono wako ulikuwa umenishikilia nisianguke

Wewe kimbilio langu

Hakuna mwingine, ni wewe pekee yako

Mbele hata nyuma, ni wewe pekee

Hakuna mwingine, ni wewe pekee yako

Mbele hata nyuma, ni wewe pekee

Tafuta tafuta hutampata kama yeye

Alinitoa toka tope la dhambi

Kama sitaona haya ya kumsifu mungu wangu

Siku zote nitamuimbia Baba

Taabu nyingi kweli nilipitia

Hadi nikajipata nikikushuku

Sikujua mpango wako kwangu Baba

Ulijua yote nikiyapitia

Mkono wako ulikuwa umenishikilia nisianguke

Wewe kimbilio langu

Hakuna mwingine, ni wewe pekee yako

Mbele hata nyuma, ni wewe pekee

Hakuna mwingine, ni wewe pekee yako

Mbele hata nyuma, ni wewe pekee

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *