Adawnage Band – Naomba

Sikudhani Mimi Nimekupa Weh, Huzuni Kiasi Hicho
Dhambi Mingi, Maombi Hayatoki Nisamehe Baba
Uchovu Na Uvivu Umenijaza, Moyoni Sina Amani

Naomba Unipe Raha, Msamaha, Mi Naomba Uwashe Taa
Popote Niendapo Chochote Nifanyacho Sasa, Nifungue Macho
Nipate Kuona, Kuhisi, Nipate Upako Wako

   Naomba Baba, Mimi Naomba, Mikono Nimeinua

   Nishike Baba, Unifiche Mikononi Mwako

   Nionyeshe Baba Wema Wako, Unifanye Chombo Chako

   Naomba, Naomba, Baba Mi Naomba

Sikudhani Mimi Nikiteleza, Nakusulubu Tena
Uchungu Mwingi, Machozi Yakutoka, Nisamehe Baba

Unizibie Ufa, Nisijenge Ukuta, Bwana Umetukua
Naomba Unipe Raha, Msamaha, Mi Naomba Uwashe Taa
Popote Niendapo Chochote Nifanyacho Sasa, Nifungue Macho
Nipate Kuona, Kuhisi, Nipate Upako Wako

   Naomba Baba, Mimi Naomba, Mikono Nimeinua

   Nishike Baba, Unifiche Mikononi Mwako

   Nionyeshe Baba Wema Wako, Unifanye Chombo Chako

   Naomba, Naomba, Baba Mi Naomba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *